Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. —WAEBRANIA 4:15
Kulingana na mwandishi wa Waebrania, Yesu alipitia kila hisia na kuteseka kwa kila hisia ambayo mimi na wewe hupitia, lakini bila kutenda dhambi. Hakutenda dhambi kwa sababu hakuzikubali hisia zake mbaya. Alijua Neno la Mungu katika kila eneo la maisha kwa sababu alitumia miaka mingi kulisoma kabla ya kuanza huduma yake. Wewe na mimi hatutaweza kusema hapana kwa hisia zetu kama hatuna maarifa makuu ya Neno la Mungu.
Mtu anaponidhuru na nihisi kwamba nimekasirika au nimevurugika, ninaomba, “Yesu, nimefurahi sana kwamba unaelewa ninachohisi sasa hivi na kwamba hunihukumu kwa kuhisi hivi. Sitaki kutoa hisia zangu. Nisaidie kuwasamehe walionikosea na nisiwashikie chuki, kuwaepuka, au kuwalipiza kisasi kwa madhara waliyonifanyia.” Haijalishi ni lini au ni vipi majaribu huja, Mungu ametuwezesha kupinga. Lakini tunahitaji kujua Neno lake na kumwegemea kwa usaidizi. Hatuwezi kufanya kwa nguvu zetu wenyewe; ni Neno lake na Roho wanaotuwezesha kupinga majaribu! Si vibaya kuhisi kujaribiwa, lakini ni vibaya tukikubali majaribu hayo.
Dhibiti hisia zako—usiache zikudhibiti!