Aliye Nawe ni Mkuu Zaidi

Aliye Nawe ni Mkuu Zaidi

Iweni hodari na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sabau ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye. 2 MAMBO YA NYAKATI 32:7

Nia ambayo mimi nawe tunaweza kuwa nayo usoni mwa shida zetu ni moja ya amani na tumaini. Badala ya kutazama makosa yetu ya nyuma, matatizo yetu yaliopo, au hofu za mustakabali wetu, tunaweza kumtazama Bwana, tukiwa na wingi wa shukrani kwa hekima, nguvu, na uwezo wake. Tunaweza kujikumbusha kwamba haijalishi ni shida ngapi zinazotukabili, Aliye nasi ni mkuu kuliko wale wote wanaotupinga.

Tukijitegemea kabisa au kuwategemea watu wengine, tunajitayarisha kushindwa na kusikitika. Kitu kizuri kabisa tunachoweza kufanya katika hali yoyote ni kumwegemea Mungu. Huenda watu wanaweza kutufeli au kutusikitisha, lakini tunaweza kushukuru Mungu kwamba hatawahi kutuacha wala kutupungukia.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba hutawahi kuniacha wala kunipungukia. Asante kwa mahusiano yaliyo katika maisha yangu, lakini nisaidie kukumbuka kuja kwako kwa kuwa usaidizi kabla sijaenda kwa mtu mwingine. Wewe ni chanzo changu cha kwanza cha usaidizi na nguvu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon