Achana na maisha ya majuto na ufanye uchaguzi mpya

Achana na maisha ya majuto na ufanye uchaguzi mpya

Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 2 Wakorintho 5:17

 Uchaguzi mbaya husababisha huzuni, na tunapopata majuto tunahitaji kukabiliana na hilo na tuiruhusu kutufundisha jinsi ya kufanya maamuzi mazuri katika siku zijazo. Ninaelewa mwenyewe kwamba uchaguzi mbaya husababisha kujuta.

Nakumbuka wakati fulani miaka kadhaa iliyopita nilipojiangalia na kuona tofauti kati ya mume wangu, Dave, na mimi, kwa sababu amefanya mazoezi maisha yake yote na ana afya, nguvu na sura nzuri ya kimwili.

Mwanzoni, nilikuwa na majuto tu kwamba sikuwa na nguvu kama Dave, lakini nilitambua kuwa naweza kufanya kitu kuhusu hilo. Sasa ninafanya mazoezi mara kwa mara na nimeshangazwa na tofauti nzuri ambayo imefanya.

Biblia inasema kuwa pamoja na Mungu, wewe ni kiumbe kipya. Huna haja ya kuishi katika njia zako za zamani, lakini sasa unaweza kufanya uchaguzi mpya, bora zaidi unaowezeshwa na Roho Mtakatifu.

Ikiwa unapata ukijutia baadhi ya uchaguzi usio wa busara uliyofanya wakati uliopita, usijidanganye katika kufikiri kuwa umechelewa sana kufanya chochote kuhusu hilo. Anza tu kufanya kilicho haki na kisha tilia mkazo kwa hilo.

Unapoanza kufanya maamuzi bora, utakuja kupata maisha ya kufurahia baraka za Mungu kila siku.

 OMBI LA KUANZA SIKU

 Roho Mtakatifu, najua kwamba nimefanywa kiumbe kipya. Sitaki kuishi katika majuto kuhusu siku za nyuma. Nisaidie kufanya uchaguzi mzuri ili nipate kufurahia siku zijazo ulizo nazo kwa ajili yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon