Huru Kutokana na Wasiwasi

Msisumbuke, basi, mkisema, tule nini? Au tunywe nini? au tuvae nini…kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. —MATHAYO 6:31–32

Wasiwasi hutujaza hofu na wasiwasi, na kutufanya tufikirie: “Je, ikiwa hatuna ya kutosha? Nitapata vipi kazi nyingine? Je, iwapo mambo hayatakuwa mazuri?” Kwa maneno mengine, “Tutafanya nini Mungu asipotusaidia?”

Badala ya kukiri ahadi za Bwana tunapohisi kukosa uhakika kuhusu kitu, mara nyingi huwa tunazungumza kuhusu wasiwasi wetu na masikitiko, jambo ambalo huyafanya yawe makubwa na kufanya zetu zionekane mbaya sana kuliko vile zilivyo.

Wasiwasi na mfadhaiko ndio watu hupitia wanapokosa kujua kwamba wana Baba wa mbinguni anayewapenda bila masharti. Lakini mimi na wewe tunajua tuna Baba wa mbinguni aliye karibu nasi na ameahidi kutupatia kila kitu tunachohitaji. Ni muhimu sisi kukumbuka hili na kutenda mambo kwa imani tukimtumainia Mungu kila siku. Eti kwa sababu tunajaribiwa kuwa na wasiwasi haimaanishi lazima tuwe nayo!

Yesu anakuhakikishia kwamba Baba yako wa mbinguni anajua mahitaji yako yote hata kabla umwombe. Kwa hivyo kwa nini uwe na wasiswasi? Badala yake, shukuru Mungu mapema kwa sababu ya vitu atakavyokupa maishani mwako.


Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake; kisha tutazidishiwa hivi vitu vyote tunavyohitaji (Mathayo 6:33).

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon