Mungu anaweza kutumia majaribio yako makubwa kwa manufaa yako

Mungu anaweza kutumia majaribio yako makubwa kwa manufaa yako

Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. Mwanzo 50:20

Mungu aliniambia kwa moyo wangu wakati fulani: Joyce, unaona mwishoni mwa pua yako (ambayo si mbali sana), na unafikiri kwamba kitu chochote ambacho hakikai sawa si nzuri. Lakini ninaona kutoka mwanzo hadi mwisho kwa sababu mimi ni Mwanzo na Mwisho, na ninajua mambo mengi ambayo hujui.

Tunajua kwa sehemu … lakini Mungu anajua yote.

Katika Mwanzo 50:20, Yusufu anazungumza na ndugu zake, ambao walikuwa wamemtendea vibaya sana. Walipomtupa shimoni na kumpeleka katika utumwa, walidhani walikuwa wakimfanyia mabaya, lakini kwa hakika, Mungu alikuwa na mpango wa kutumia majaribio hayo ili kukuza Yusufu kuwa mahali pa ushawishi mkubwa.

Wakati mwingine mambo tunayofikiri ni mabaya huwa baraka kubwa. Jaribio kubwa linaweza kuendeleza ndani yako imani kuu zaidi. Unaweza kuwa chini kabisa, lakini Mungu ana mpango wa kutumia hali hiyo kukukuza katika wito Wake kwenye maisha yako.

Kumbuka, Mungu anaweza kuona yote, na Yeye atatumia majaribio hayo kwa faida yako.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, siwezi kuona “kupita pua langu,” lakini ninakuamini kwa sababu najua unaona yote. Ninaamini Unaweza kuchukua majaribio yangu na kuleta mazuri kutokana nayo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon