Ishara Nyekundu, Ishara ya Kijani Kibichi

Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani ya andiko (WARUMI 7:6)

Kumekuwa na nyakati katika maisha yangu ambazo sikuwa na furaha, hata ingawa nilikuwa Mkristo na kufanya kila kitu ambacho nilifikiri Mkristo alifaa kufanya. Ninatazama nyuma sasa na kugundua mojawapo ya sababu kuu za kutokuwa na furaha ni kwamba sikujua mengi kuhusu maisha ya ndani. Sikujua jinsi ya kusikiliza sauti ya Mungu ikinielekeza kutoka ndani kwa nguvu za Roho Mtakatifu au jinsi ya kumtii aliponichochea kufanya au kutofanya vitu vingine.

Sasa Roho Mtakatifu hutenda kama askari wa trafiki ndani yangu. Ninapofanya vitu kwa njia iliyo sawa, ninapata mwanga wa kijani kibichi kutoka kwake, na ninapofanya vitu visivyo sawa, ninapata mwanga mwekundu. Nikikaribia kujiingiza mashakani, lakini niwe sijachukua msimamo kabisa ninapata ishara ya tahadhari.

Kadri tunavyosimama na kumwomba Mungu uelekezi ndivyo tunakuwa wahisivu zaidi kwa ishara za ndani ambazo Roho Mtakatifu hutupatia. Hutuzungumzia kwa sauti tulivu ndogo au ninachoita “kujua.” Sikiliza ishara zenye upole za Roho Mtakatifu katika utu wako wa ndani jinsi tu unavyoweza kuzingatia mianga miekundu na ya kijani kibichi unapoendesha katika trafiki. Ukipata mwanga wa kijani kibichi, basi endelea kwenda; na mwanga ukiwa mwekundu, simama!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Ukiwa katika maeneo mapya, tumia ishara za Mungu za maombi.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon