Jema kutokana na Baya

Jema kutokana na Baya

Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. —MWANZO 50:20

Mungu anataka kurejesha nafsi yako. Kadri unavyomkaribia, ndivyo unavyoshuhudia zaidi uponyaji, nguvu na nguvu za zake za urejesho. Atakuregesha mahali ambapo maisha yako yaliondokea katika njia na kusawazisha kila kitu kuanzia wakati huo na kuendelea.

Yusufu ni mfano wa kale wa kibiblia kuhusu vile Mungu huchukua kilichokusudiwa kuwa kiovu dhidi yetu na kukigeuza kufanya kazi kwa ajili ya wema wetu. Katika onyesho hilo la vioja, ambapo Yusufu anasema katika Mwanzo 50:20, anawaambia ndugu zake kwamba uovu waliokusudia kumtendea (na ulikuwa uovu kweli), Mungu alikuwa ameutumia kwa wema kuwaokoa pamoja na familia zao na mamia ya maelfu ya watu katika msimu wa njaa.

Katika maisha yangu binafsi, siwezi kusema kwa ukweli kuwa nina furaha kwamba nilidhulumiwa. Lakini kupitia kwa nguvu za msamaha na kumpa Mungu uchungu wangu, ameniponya na kunifanya kuwa mtu bora, mwenye nguvu, mwenye nguvu zaidi za kiroho na kuwa macho kwa mambo ya kiroho. Ameirejesha nafsi yangu na kuondoa woga na hisia za kutokuwa salama. Ninaweza kuamini, kupenda, kusamehe, na kuishi maisha rahisi kutokana na mtazamo wangu wa maisha kwa sababu Mungu amerejesha nafsi yangu, na anaweza kukufanyia vivyo hivyo.


Iwapo vitu vibaya vimefanyika katika maisha yako, kumbuka hili: Ni Mungu peke yake anayeweza kurejesha hali yako. Anaweza kuleta jema kutokana na baya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon