Kukabili Hofu Kwa Maombi

Kukabili Hofu kwa Maombi

Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; mwanadamu atanitenda nini? —Waebrania 13:6

Hofu hushambulia kila mtu. Ni njia ya adui ya kujaribu kutuzuia kufurahia maisha ambayo Yesu alikufa ili kutupatia. Tukikubali hofu na kuitamka, tunafungua mlango kwa adui na kufunga mlango kwa Mungu.

Lakini badala ya kukubali hofu, tunaweza kujifunza kukiri kwa ujasiri kwamba Mungu ni Msaidizi wetu, Kimbilio letu, na Ngome yetu.

Biblia inatufundisha kukesha na kuomba. Mathayo 26:41: inasema “Sisi sote tuwe macho, (tusikilize kwa makini, tuwe waangalifu na wenye kujishughulisha) na kukesha na kuomba, kwamba usije kuingia katika majaribu. Kwa kweli roho anataka, lakini mwili ni mnyonge.” Marejeleo muhimu katika kifungu hiki ni kujitunza na mashambulizi ambayo adui huanzisha dhidi ya nia zetu na hisia zetu. Mashambulizi haya yanapotambuliwa, tunaweza kuomba mara moja. Ni wakati ule tunaoomba ndipo nguvu huachiliwa katika maisha yetu- sio tunapofikiria kuomba baadaye.

Ninakuhimiza kukesha na kuomba kuhusu kila kitu. Ninaamini utapata huu uamuzi ukiwa wa kuzalisha furaha zaidi na amani kwa maisha yako ya kila siku.


Ili kuishi katika ushindi wa kweli, ni muhimu kujiweka wakfu katika maombi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon