Chagua mawazo bora na uwe na maisha bora

Chagua mawazo bora na uwe na maisha bora

Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. Mithali 18:21

Andiko hili linasema wazi kwamba mauti na uzima huwa katika maneno tunayosema. Ni muhimu sana kujifunza kudhibiti vinywa vyetu, lakini tunahitaji kuhakikisha tunafanya kwa njia sahihi. Nadhani watu wengi wanajaribu kudhibiti vinywa vyao lakini hawafanyi chochote kuhusu mawazo yao. Hiyo ni kama kuondoa magugu – mizizi isipo shughulikiwa, magugu yanarudi tena. Huwezi kamwe kudhibiti kinywa chako isipokuwa kwanza ujifunze kudhibiti akili yako.

Mara nyingi tunajaribiwa kufikiri mawazo mabaya, lakini hatupaswi kukubaliana nayo. Tuna uchaguzi! Tunaweza kuchagua kwa uamuzi kufikiri vizuri ili tuweze kuchagua kuzungumza mambo mema. Unaweza kuchagua mawazo ya kuzalisha maisha kwa kusikia, kusoma, kufikiri na kuzungumza juu ya Mungu na Neno Lake. Kile kilicho ndani yako kitapata njia yake nje, hivyo wakati unapojaza akili yako kwa vitu vyema, vyenye nguvu, vya uzima kutoka kwa Mungu, maneno yenye nguvu, yenye afya, yanayotoa maisha yatakufuata kwa kawaida.

OMBI LA KUANZA SIKU

Roho Mtakatifu, nataka kubadili mawazo yangu ili niweze kuzungumza maneno ya uzima. Nisaidie kufanya upya mawazo yangu kwa Neno lako ili maneno yangu yakuonyeshe Wewe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon