Kusahau kuhusu sisi wenyewe

Kusahau kuhusu sisi wenyewe

Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. Wagalatia 2:20

Paulo alisema kuwa amesulubiwa na Kristo. Kwa maneno mengine, alikuwa ameacha kufikiri juu yake mwenyewe ili kuishi kwa ajili ya Mungu. Na tunahimizwa kufanya sawia.

Katika hatua hii unaweza kuwa unafikiri, Na mimi je? Ni nani atakayejali mimi? Hii kwa kawaida hutuzuia kuishi kama Mungu anavyotaka tuishi. Ni rahisi kufikiri tu juu ya kile tunachotaka, kufikiri na kujisikia, lakini kuishi kwa ajili yako mwenyewe ni njia ya kukata tamaa, na kuishi kwa utupu. Ni ajabu jinsi kulenga Mungu na kile tunachoweza kufanya kwa wengine huleta uhuru kutokana na hofu ya kuwa na kile tunachohitaji au tunachotaka.

Siri ya kuwa na furaha ni kutoa maisha yako badala ya kujaribu kuyaweka. Unapotoa mtazamo kwako na kumzingatia Mungu, anaweza kukuonyesha jinsi ya kuishi maisha yenye maana. Ninakuhimiza kuanza siku zako kwa kujitolea kwa Mungu. Wakati unapofanya hivyo, Yeye atakusaidia kwa uaminifu kuishi maisha ya kimungu

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nakupa macho yangu, masikio, kinywa, mikono, miguu, moyo, fedha, zawadi, talanta, uwezo, wakati, nishati- yangu yote! Sitaki kuishi kwa ajili yangu-nataka kuishi kwa ajili yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon