Muite Mungu “Abba”

Muite Mungu "Abba"

Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Warumi 8:15

 Hofu inaweza kuwa na ushawishi mkubwa katika maisha yetu, lakini ukweli ni kwamba ni hali ya adui kupotosha  imani. Anatuambia: “Amini kile ninachokuambia. Hii haitafanya kazi. Sala zako sio nzuri hata kidogo. Huna haki ya kusimama mbele ya Mungu. Wewe umeshindwa. ”

Hofu daima inakuambia kile usichokuwa, kile huna, kile huwezi kufanya na kile hutawahi kuwa kamwe. Lakini Warumi 8:15 inasema kwamba wewe ni mtoto wa Mungu ambaye unaweza kumwita “Abba Baba.”

Neno Abba lilikuwa la watoto kwa muda mrefu ambalo lilitumiwa kuwaita baba zao. Ingekuwa sawa na neno letu “Daddy.” Sio rasmi zaidi kama Baba ila linaashiria ukaribu  kati ya mtoto na baba yake.

Yesu alisema tunaweza kumwita Mungu “Abba” kwa sababu Yeye alituokoa kutokana na hofu yote. Yeye atawajali watoto wake wapendwa daima, na tunaweza kumkaribia Yeye bila hofu ya kukataliwa. Tunapokimbia kwake kwa tatizo lolote au maumivu, Yeye anasubiri kwa mikono ya wazi ili kutufariji na kututia moyo.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Abba Baba, asante kwa kunifanya mtoto wako. Najua kwamba Wewe utanijali, kwa hivyo sihitaji kuishi katika utumwa wa hofu. Nakupenda!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon