Kutafuta Mapenzi ya Mungu

Kutafuta Mapenzi ya Mungu

Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. WAEFESO 5:17

Wingi wa Wakristo hutaka kujua mapenzi ya Mungu juu ya maisha yao. Hebu niwaeleze angalau sehemu ndogo ya mapenzi ya Mungu ni nini? Siwezi kukwambia iwapo mapenzi yake juu yako ni wewe kuhamia Minneapolis au la, au mahali utawapeleka watoto wako shule, au kama wewe ndiwe unafaa kupata nafasi ya mhusika mkuu katika mchezo wa pasaka kanisani. Lakini ninaweza kukupa njia ya hakika kabisa ya kujua na kutii mapenzi ya Mungu katika maisha yako: Kuwa mwenye shukrani nyingi.

Kuwa mwenye shukrani—kila wakati, bila kujali unayoyapitia. Hilo ni sawa; dumisha tu moyo wenye shukrani katika kila hali. Wakati mwingine kutoa shukrani huja kwa urahisi huku nyakati zingine ikiwa vigumu, lakini iwapo utajenga na kudumisha nia ya kutoa shukrani, utakuwa ndani ya mapenzi ya Mungu. Nitawezaje kuwa na hakika? Kwa sababu 1 Wathesalonike inasema, “Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” (BIBLIA).


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba hata nikiwa ninangoja mambo mahsusi kuhusu mapenzi yako juu ya maisha yangu, ninaweza kujua mapenzi yako mapana juu ya maisha yangu—kuwa mwenye shukrani wakati wote. Leo ninachagua kuishi ndani ya mapenzi yako kwa moyo wenye shukrani, na ninajua utafunua makusudi yako juu ya maisha yangu ya kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon