Maneno Mazuri

Mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu (WAEFESO 5:19)

Tafsiri ya Mfalme Yakobo inatafsiri andiko la leo: “ he King James Version translates today’s verse: “Mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu.” Ninapenda kutumia andiko hili kwa njia mbili. Jinsi ninavyojizungumzia ni muhimu, na jinsi ninavyozungumzia wengine ni muhimu pia.

Ni rahisi kuanguka kwenye mtego wa kuzungumza vitu hasi, matatizo, masikitiko, na hali ngumu. Lakini mojawapo ya hayo hutusaidia kukaa tukiwa tumejawa na Roho na hayaakisi yale ambayo Roho anataka kutuzungumzia kwa sababu hana uhasi kwa njia yoyote ile. Hata akituzungumzia kuhusu tatizo, huzungumza ili alete suluhu; na anapotuzungumzia kuhusu hali ngumu, anafanya hivyo ili kutuletea utulivu na nguvu. Kadri tunavyofikiria na kuzungumza kuhusu matatizo yetu, ndivyo tunavyokuwa wadhaifu lakini tunatiwa nguvu tunapozungumza na kufikiria kuhusu Yesu na ahadi zake kwetu.

Maisha si rahisi kila wakati; huwa sote tunakabiliana na hali ngumu wakati mwingine. Mungu ametujaza na Roho wake ili kutuwezesha kufanya vitu vigumu kwa urahisi. Unapopitia wakati mgumu, tega sikio lako lisikie sauti ya Mungu. Zungumza vitu chanya ambavyo Mungu husema kukuhusu katika Neno lake na kupitia kwa sauti ya Roho ndani ya moyo wako. Sisi wote hula kutoka kwa maneno yetu wenyewe kwa hivyo ni muhimu kuzungumza maneno mazuri yenye uzima teletele.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Chagua maneno yako kwa hekima leo, kwa kuwa yana nguvu za uhai au mauti.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon