Kuza Uwezo Wako Na Ufanye Jambo Sasa Hivi

Kuza Uwezo Wako Na Ufanye Jambo Sasa Hivi

Kila mfanyacho,fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu. Wakolosai 3:23

Unaweza kujua kwamba Mungu amekuumba na uwezo fulani, lakini haiishi hapo. Lazima ukuze uwezo wako.

Ninaamini kwamba watu wengi hawana furaha kwa sababu hawakuzi uwezo wao. Ikiwa ungependa kuona uwezo wako ukikua kwa njia ya ajabu, usisubiri hadi kila kitu kiwe sawa. Anza kwa kutenda chochote kile kilicho mbele yako.

Lazima uupatie uwezo wako umbo fulani kwa kutenda jambo fulani. Ikiwa una shauku ya kujaribu kitu kipya, basi chukua hatua na uone ikiwa Mungu amekupa kipawa kukitenda.Kamwe hautajua kile unachoweza kutenda ikiwa hutajaribu kitu chochote.

Ningependa kukuhimiza uushinde uoga unaojitokeza kila unapotaka kujaribu kitu kipya. Upendo wa Mungu mkamilifu huondoa uoga wote, kwa hivyo hatufai kuishi katika hofu ya kufanya makosa. Na huenda kusalia katika mazingira uliyozoea ikapendeza lakini kamwe hutaweza kuishi katika uwezo wote ulio ndani yako na pia hutaridhika katika yale unayotenda. Kwa hivyo kata kauli kutoka nje na kutenda kile unahisi moyoni kwamba Mungu anataka ufanye.

Umejaa uwezo wa kiungu ndani yako,na Mungu anataka kutenda mengi kukupitia zaidi ya mawazo yako,lakini inahitaji ushirikiano wako. Chukua hatua, na umtumikie kwa moyo wako wote siku ya leo!


OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, katika yote ninayofanya, ningependa kukutumikia kwa moyo wangu wote. Asante kwa kunihimiza kutoka nje na kuchukua hatua, huku nikikuza uwezo wote ulioweka ndani yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon