kupata kile usichostahili

kupata kile usichostahili

Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu. Zaburi 40:1-2

Watu wengi wanaruhusu Mungu kuwasaidia tu wakati wanafikiri wanastahili. Wakati mmoja katika maisha yangu nilikuwa hivyo. Kwa miaka mingi niliona kwamba Mungu anapaswa kunisaidia tu wakati nilifikiri kuwa nimestahili, wakati nilifikiri nimefanya matendo mema ya kutosha ili kustahili msaada Wake.

Aina hiyo ya kufikiri haiwezi kuzalisha mtazamo wa shukrani. Ikiwa tunadhani tunastahili kile tunachokipokea, basi sio zawadi bali malipo au “malipo ya huduma zinazotolewa.” Tofauti kati ya kupokea kile hatustahili na kupokea kile tunachostahili ni tofauti kati ya neema na kazi. Ninakuhimiza kufungua moyo wako na kuruhusu neema ya Mungu kuingia katika maisha yako kukusaidia katika kutembea kwako kila siku.

Daima kumbuka kwamba unapofadhaika, ni kwa sababu unaishi kwa jitihada zako na kuna haja ya kurudi katika neema ya Mungu kwa kumruhusu kufanya kazi kupitia kwako.

Jifunze kumruhusu Mungu akusaidie, acha kujaribu kustahili msaada wa Mungu na kumruhusu akutane na mahitaji yako yote.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, mimi natambua upumbavu wa kukubali tu msaada wako wakati najisikia kama anayestahili. Ninaachana na kazi zangu na kupokea neema yako. Asante kwa kunisaidia katika kila hali, hata wakati sipaswi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon