Msafishaji Wetu

Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha (MALAKI 3:3)

Ninapoangalia nyuma katika miaka iliyopita, ninaweza kuona kwamba nimekuwa katika safari ya kuvutia na Mungu. Bila shaka amenibadilisha na angali ananibadilisha kila siku. Nilikuwa na matatizo mengi sana katika nafsi (nia yangu, hiari, na hisia) yangu na katika hali zangu wakati huo, nilipokea ukamilisho wa Roho Mtakatifu. Sikujua kabisa kile ambacho kilikuwa karibu kufanyika katika maisha yangu. Nilikuwa ninamwomba Mungu mabadiliko, lakini sikujua kabisa kwamba kilichohitajika kubadilika katika maisha yangu kilikuwa mimi!

Mungu akaanza mchakato ndani yangu- polepole, kwa umadhubuti, na kila mara kwa mwendo ambao ningestahimili. Kama msafishaji anakaa juu ya mioto ambayo huchoma katika maisha yetu ili kuhakikisha haiwi moto sana na kwamba haizimi kamwe. Wakati tu ule ambao anaweza kutuangalia na kujiona ndivyo inakuwa salama kuuzima moto huo, na hata hivyo huwa tunaendelea kuhitaji mabadiliko machache wakati mwingine.

Mungu alipokuwa akinishughulikia kuhusu subira, nilikabiliana na hali nyingi ambamo ningekuwa mwenye subira au nikawa mbaya kitabia. Mara nyingi, tabia zangu hazikupendeza, lakini Roho Mtakatifu akaendelea kunithibitisha, kunifundisha, na kunipa matamanio ya kuishi kwa sababu ya utukufu wa Mungu. Kwa utaratibu, pole pole, nilibadilika katika eneo moja, halafu jingine. Mara nyingi nilipumzika kidogo katikati ya vita na mara nyingi kufikiria kwamba, labda nilikuwa nimefuzu mwishowe, hadi nilipogundua kwamba kuna kitu kingine nilichohitaji kujifunza.

Hivyo ndivyo inavyofanyika Roho Mtakatifu anapotubadilisha. Fungua moyo wako kwa uongozi wake; fungua masikio yako kwa sauti yake; tii anachokuambia- na hivi karibuni, utajipata ukibadilika zaidi na zaidi hadi kuwa mtu aliyekuumba kuwa.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usikate tamaa Mungu anapokuonyesha maeneo ndani yako yanayohitaji mabadiliko.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon