Usitafakari juu ya masikitiko madogo

Usitafakari juu ya masikitiko madogo

Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako. Zaburi 119:15

Dhiki kubwa haitokani na masikitiko makubwa, kama tunaposhindwa kupata kazi au kupandishwa cheo tulichotaka. Maumivu makubwa ya kihisia yanaweza kutokea kwa mfululizo wa machungu madogo na kuumia. Ndiyo sababu tunapaswa kujua jinsi ya kushughulikia masikitiko madogo, kila siku na kuyaweka kwa mtazamo.

Unapozingatia kitu daima, kinaitwa kutafakari. Vikwazo vidogo vinavyokuja kila siku vinasumbua, lakini wakati vinapoingia, huenda ikaonekana haiwezekani kutafakari kitu kingine chochote.

Lakini badala ya kuzingatia matatizo yako na kukata tamaa, mfikirie Mungu na utafakari ahadi zake kwa ajili yako. Maisha yanaweza kukuweka chini, lakini haufai kubaki hapo. Mungu yuko tayari, na anaweza kukuchukua.

Wakati masikitiko yanakulemea, unaweza kuyaruhusu yakugandamize, au unaweza kutumia kama hatua ya kuendelea katika mambo mazuri. Chagua kukumbana na masikitiko wakati yanapoanza kwa kutafakari juu ya njia za Mungu. Ana mambo mazuri kwako, naye atakusaidia kushinda masikitiko hayo

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, kama vile Zaburi 119:15 inavyosema, nitatafakari juu ya Neno lako, sio shida kidogo ambazo zinajaribu kuniweka chini. Neno lako lina nguvu na linatoa maisha, kwa hiyo najua ninaweza kushinda masikitiko kwa kukuangalia Wewe!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon