Neema na Neema Zaidi

Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. —Yakobo 4:6

Wanadamu wote wana mielekeo ya uovu, lakini Yakobo anatufundisha kuwa Mungu atatupatia neema na neema zaidi ya kushinda mielekeo hii.

Nilitumia muda mwingi wa maisha yangu ya Kikristo nikijaribu kushinda nia na dhamira zangu mbaya. Lakini kujaribu kwangu kote kulileta tu masikitiko zaidi. Ilinilazimu kuja mahali pa unyenyekevu na kujifunza kwamba Mungu hutoa neema kwa wanyenyekevu—sio wenye kiburi. Anawapa usaidizi walio wanyenyekevu kiasi cha kuuitisha.

Tuna mawazo yetu binafsi kuhusu tunayoweza kutimiza, lakini mara nyingi huwa tuna mawazo makuu kujihusu kuliko inavyopasa. Tunafaa kuwa na fikra za unyenyekevu, tukijua kwamba bila Mungu, hatuwezi lolote.

Iwapo una mipango yako, kujaribu kufanya vitu vifanyike kwa nguvu za mwili wako, basi utasikitika. Pengine umesema, “Hata nikifanya nini, hakuna kinachofanyika!” Hakuna kitakachowahi kufanyika hadi ujifunze kutumainia neema ya Mungu.

Tulia. Acha Mungu awe Mungu. Acha kujiwia mgumu. Mabadiliko ni mchakato unaokuleta karibu naye polepole. Uko njiani, kwa hivyo furahia safari.


Iwapo unatamani kuwa huru, kuwa tayari kubadilisha jitihada za mwanadamu na kumwamini Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon