Nguvu Ya Makubaliano

Nguvu ya Makubaliano

Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake. —Matendo Ya Mitume 1:14

Waaminio wanapoungana katika maombi, huwa kuna nguvu kuu. Yesu mwenyewe alisema, “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” (Mathayo 18:20).

Katika kitabu kizima cha Matendo ya Mitume, tunasoma kwamba watu wa Mungu walikusanyika pamoja kwa “moyo mmoja” (Matendo ya Mitume 2:1, 46:4, 4:24, 5:12, 15:25). Na ilikuwa imani yao ya umoja, makubaliano ya ushirika, na upendo ambavyo vilifanya maombi yao kuwa na matokeo sana. Waliona Mungu akitenda mambo makuu kuthibitisha ukweli wa Neno lake huku wakitoa ushuhuda kwa imani yao.

Kuishi katika makubaliano hakumaanishi kwamba tuhisi kwa njia moja sisi sote kuhusu kila kitu, lakini inamaanisha kwamba tumekusudia kutembea katika upendo. Tunaweza kuheshimu maoni ya mtu hata kama hatukubaliani nayo! Mimi na Dave huwa hatukubaliani kuhusu mambo mengi, lakini tunaishi kwa amani na kuelewana na hutupatia nguvu katika maombi.

Katika Wafilipi 2:2 tumeambiwa na Mtume Paulo, ijalizeni furaha yangu, muwe na nia moja…”

Maombi ni faida ya ajabu, na ambayo tunafaa kufanya kila mara. Lakini ili tuwe na matokeo mazuri, tunafaa kung’ang’ana kuondoa kutoelewana na kutoungana katika maisha yetu.


Kuwa katika makubaliano mara nyingi huwa muhimu kuliko kuwa sahihi!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon