Nguvu za Furaha na Amani

Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba angurumaye, huzungukazunguka, akitafuta mtu ammeze. —1 PETRO 5:8

Ukijipata katika hali inayotatiza, acha lengo lako liwe kuwa mtulivu tu. Kila wakati unapoanza kukasirika au kusikitika, acha na ujiulize, “Adui anajaribu kufanya nini hapa?”

Kama shatani hatakusukuma kuwa na woga na kukasirika kuhusu shida, hatakuwa na nguvu juu yako. Unabaki katika nguvu na uwezo wa Mungu ukidumisha fikra tulivu, zenye amani na kutumainia.

Roho Mtakatifu hufanya kazi katika mazingira ya furaha na amani. Hafanyi kazi katika fujo. Katika wakati wa majaribu, nguvu zako zinapatikana katika kumkaribia Mungu na kuingia katika utulivu wake. Haya maneno yote ya kibiblia kama—kaa, utulivu, raha, simama, na ndani ya Yesu—kimsingi yanasema jambo moja: Usipoteze furaha na amani yako.

Ndani ya Kristo, umeitwa kuwa mshindi. Una hakikisho la kuwa mshindi ndani yake wakati wote. Ukishughulikia kila shida inavyokuja, itasuluhishwa hatimaye. Yesu huwa nawe daima katika kila hali. Kumbuka tu kumtumainia kwa furaha na amani ya leo.


Kuna nguvu kuu katika kuchagua kutembea katika amani na furaha, bila kujali hali zinazokuzingira.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon