Njia bora ya kukabiliana na pesa

Njia bora ya kukabiliana na pesa

Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu;  Mithali 28:27

 Nimegundua njia bora ya kukabiliana na pesa ni kuitoa. Na tunahitaji kuendelea kutoa, hasa wakati wa changamoto za kifedha. Hili ni jambo muhimu katika kutusaidia kudumisha mtazamo wa Biblia juu ya fedha zetu. Daima inawezekana kuishi kwa kanuni za kifedha za Mungu, hata wakati wa magumu.

Huenda ukajikuta katika kile kinachoonekana kama hali isiyowezekana ya kifedha na kujisikia kama huna nafasi ya kutoa, lakini usiruhusu hilo likuzuie. Mungu atakusaidia wakati unapofanya kazi na kile ulicho nacho.

Luka 19:17 inatuambia kwamba Mungu anafurahi wakati sisi ni waaminifu na wa kuaminiwa katika mambo madogo sana. Tukiwa hivyo, inasema atatupa mamlaka juu ya mambo makuu.

Mithali 28:27 inasema, Yeye anayewapa maskini hatakosa… Ikiwa tutamtii Mungu kwa fedha zetu, hata wakati hatuna mengi, na kuwapa watu wengine, Mungu atatupa kile tunachohitaji. Ni rahisi sana. Chagua kuwa mtoaji leo, na huwezi kukosa chochote.

 OMBI LA KUANZA SIKU

 Mungu, ninachagua leo kutoa fedha zangu kwako. Hata katika nyakati ngumu, najua kanuni zako za kifedha zinafanya kazi na Wewe utaniangalia. Wewe ni Chanzo changu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon