Shikilia Kwa Ustahimilivu

Shikilia kwa Ustahimilivu

Tena tusichoke katika kutenda mema, maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. —WAGALATIA 6:9

Katika Wagalatia 6:9, “kukata tamaa” na “kuzimia” yanamaanisha kukata tamaa katika fikra. Roho Mtakatifu anatuambia tusikate tamaa katika fikra zetu, kwa sababu tukiendelea kushikilia, tutavuna mema hatimaye.

Fikiria kuhusu Yesu. Punde tu baada ya kubatizwa na kujazwa na Roho Mtakatifu, aliongozwa hadi nyikani kujaribiwa na Ibilisi. Hakulalamika, kukata tamaa wala kufadhaika. Hakuwaza wala kuzungumza kwa uhasi. Hakuchanganyikiwa akijaribu kufikiria kwa nini hayo yalifanyika. Alipitia kila jaribu kwa ushindi (Luka 4:1-13).

Unaweza kumfikiria Yesu akisafiri nchini, akizungumza na mitume kuhusu vile kila kitu ni kigumu? Unaweza kumpiga picha akijadili vile msalaba utakuwa mgumu… au vile alivyoogopa mambo yanayokuja… au vile alivyosikitika kwa kukosa nyumba, kitanda cha kulalia usiku?

Yesu alitoa nguvu kutoka kwa Baba yake wa mbinguni na akaondokea kuwa mshindi. Tuna Roho wake anayeishi ndani yetu na nguvu zilizopo kutufanya tushinde hali zote tunazokabiliana nazo.


Tunaweza kukabiliana na hali zote vile Yesu alifanya—kwa kuwa tayari kimawazo kupitia kwa “kuwaza ushindi” badala ya “kuwaza kukata tamaa.”

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon