Kufanya uamuzi wa kusamehe

Kufanya uamuzi wa kusamehe

Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.  —Marko 11:25

Mtu anapotuumiza moyo, mara nyingi huonekana kama mtu huyo ameiba kutoka kwetu. Tunasikia kwamba wana deni kwetu, lakini Mungu anataka tuyaache.

Ikiwa tunakataa kusamehe, tuna tumaini gani la kupokea kile tunahitaji? Kupokea kutoka kwa Mungu kile alichoahidi katika Neno Lake, tunapaswa kumtii, bila kujali ni vigumu kiasi gani. Lazima tusamehe.

Udanganyifu mkubwa zaidi ambao Shetani ameendeleza katika eneo la msamaha ni wazo kwamba ikiwa hisia zetu hazibadiliki, hatujasamehe kweli. Unapoamua kumsamehe mtu, usiruhusu shetani akushawishi kuwa kwa sababu bado una hisia zile zile, hukumsamehe mtu huyo.

Unaweza kufanya uamuzi sahihi wa kusamehe na “usijisikie” tofauti yoyote. Hapo ndipo imani inapoingia. Umefanya sehemu yako-sasa umngojee Mungu. Atafanya sehemu Yake na kuponya hisia zako, kukufanya uzima, na kubadilisha hisia zako kwa mtu aliyekuumiza.


Ombi La Kuanza Siku

Bwana, nachagua kuwasamehe wale walioniumiza moyo. Ninawaachilia kutoka kwa madeni yao, kwa jina la Yesu. Ponya moyo wangu na unifanye mkamilifu tena.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon