Kutoa yote kwa Mungu

Kutoa yote kwa Mungu

Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya. Mithali 3:9-10

Watu wengi wanataka kupokea kutoka kwa Mungu, lakini hawana nia ya kujitoa wenyewe kwake. Kweli , ni vizuri kwetu sote kutathmini maisha yetu na hali ya mioyo yetu mara nyingi kutusaidia kukaa makini katika Mungu, tuwe tayari kutoa na kufanya yote anayoweka ndani ya mioyo yetu kufanya. Na kutakuwa na nyakati tunapohitaji kujitolea na kujipeana wenyewe, wakati wetu, na pesa zetu katika kazi ya Bwana.

Usimruhusu shetani akuongoze kutokana na kutoa kwa mawazo ya uoga. Yesu anatuhimiza tusiwe na wasiwasi au hofu juu ya chochote, kwa maana Mungu anajua mahitaji yetu na anaahidi kututunza (ona Mathayo 6: 25-34).

Mithali 3: 9-10 inasema, Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.
Unapompa Mungu yako yote, atakuwa mwaminifu kukuhudumia. Jipeane mwenyewe kwa Mungu. Mpe kila kitu ulicho, kila kitu unachotaka kuwa, ndoto zako zote, maono, matumaini na tamaa.

Fanya kila kitu chake, naye ataonyesha nguvu zake kupitia maisha yako. Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya. Mithali 3:9-10


OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, leo ninakupa yangu yote: mikono yangu, kinywa changu, mawazo yangu, mwili wangu, fedha zangu na wakati wangu. Kila kitu nilicho nacho ni chako. Ninataka kufanya mapenzi yako leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon