Suala la Kulenga

Suala la Kulenga

Tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu.. WAEBRANIA 12:2 BIBLIA

Ni muhimu sana kulenga kwenye vitu vilivyo sahihi. Hii ndiyo kwa sababu Neno la Mungu linatufundisha kutotazama yote yanayotuondoa katika njia na kumtazama Yesu, ambaye ni mwanzilishi na mkamilishi wa imani yetu

Chochote kile tunacholenga kufikiria hufanywa kuwa kikubwa katika mawazo yetu. Tukilenga kufikiri kuhusu matatizo yetu, tunaendelea kuyazungushazungusha katika mawazo yetu , ambayo ni kama kutafakari juu ya matatizo hayo. Kadri tunavyofikiri na kuzungumza juu ya matatizo yetu, ndivyo yanavyokuwa makubwa zaidi. Jambo dogo linaweza kuwa kubwa kwa sababu tunalifikiria sana.

Badala ya kutafakari juu ya matatizo yetu, tutakuwa na hekima kutafakari juu ya Neno la Mungu na ahadi zake kwa maisha yetu na kumshukuru kwa hayo. Tutakapofanya hivyo, tutaona uaminifu wa Mungu ukifunuliwa, na hata hivyo, matatizo yetu hayataonekana makubwa.


Sala ya Shukrani

Nina shukuru, Baba, kwamba wewe ni mkubwa kuliko matatizo yangu, majaribu na wasiwasi. Wewe ni mwema na moyo wangu umejaa shukrani kwako na upendo wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon