Ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu katika Kristo. Filemoni 1:6
Unapojua ukweli wa kimaandiko ufuatao, huwezi kuacha kuwa na shukrani…
Tunajua kwamba sisi ni wana wa Mungu, na kwamba tumeitwa, kupakwa mafuta, na kuteuliwa naye kuwa wakuu. Tulichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake kuleta utukufu kwa Mungu na kufinyangwa kwa mfano wa Yesu Kristo. Tuna (sio tutakuwa nayo) haki, amani, na furaha ndani ya Roho Mtakatifu. Tumesamehewe dhambi zetu zote—hata zile ambazo hatujatenda bado—na majina yetu yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo. Yesu ametangulia mbele yetu kutuandalia mahali, ili alipo yeye, tuwe hapo naye pia.
Tunajua kwamba hadi arudi kutuchukua, amemtuma Roho Mtakatifu wake kama hakikisho letu la vitu vizuri vinavyokuja. Tumehakikishiwa urithi, kwa kuwa tulinunuliwa kwa damu ya Yesu Kristo. Tuna agano jipya na tumepewa njia mpya ya kuishi!
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru leo, Baba, kwa hizi ahadi ambazo ninaweza kutangaza kwa mamlaka ya Andiko. Ninajua kwamba mimi ni wako na hakuna mtu yeyote au kitu chochote kinachoweza kunitenganisha na upendo wako. Asante kwa hakikisho lako.