Uchukua hatua kwa uhuru wako

Uchukua hatua kwa uhuru wako

Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.  Yohana 8:36

Kwa kuwa Mungu hakutuumba tuishi katika utumwa wa aina yoyote, tunaweza kupata uhuru-uhuru wa kufurahia yote ambayo Mungu ametupa katika Kristo. Yeye ametupa uzima, na lengo letu linapaswa kuwa kufurahia.

Katika maisha yetu, hatuwezi tu kutamani kuwa huru. Tunapaswa kuchukua hatua. Ni muhimu kwetu kutii Neno la Mungu na kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu. Hii inamaanisha hatuwezi tu kusikia au kusoma Neno ili kupata matokeo – tunahitaji pia kufanya kile linachosema.

Je, unafurahia uhuru katika maisha yako? Naomba kwamba Mungu atakuhimiza kutafuta uhuru ambao ni wako ndani ya Yesu. Kwa sababu alikufa msalabani ili kutuweka huru kutoka nguvu za dhambi, wewe na mimi tunaweza kuwa huru kutoka kila tatizo katika maisha.

Uhuru ni wako, sasa toka nje na uuchukue. Fuata Roho Mtakatifu na uwe huru kufurahia yote ambayo Mungu aliyo nayo kwa ajili yako katika Kristo Yesu.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, ninapata uhuru wangu kutoka kwa dhambi, utumwa na ukandamizaji wa aina yoyote ndani yako. Ninaamua kuchukua hatua kwa uhuru wangu kwa kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon