Ufunguo wa Mombi Yenye Mafanikio

Ufunguo wa Mombi Yenye Mafanikio

Siwaiti tena watumwa kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. YOHANA 15:15

Mojawapo ya funguo muhimu za maombi yenye mafanikio ni kumkaribia Mungu kama rafiki. Tukienda kwake Mungu tukiamini kwamba anatuona kama rafiki zake, maajabu mapya yanafunguliwa kwetu. Tunakuwa na uhuru mpya na ujasiri, ambavyo vyote ni vitu vya kushukuru kwavyo.

Ikiwa hatumjui Mungu kama rafiki, tutalegea kuwa wajasiri katika kuomba tunachohitaji. Lakini tukimwendea kama rafiki yetu, bila kupoteza heshima kwake, maombi yetu yatabaki mapya kila wakati, yenye kusisimua na ya undani.

Urafiki huhusisha kupenda na kupendwa. Ina maana kujua kwamba Mungu yuko upande wako, akitaka kukusaidia, akikushangilia, na mara yote akijali maslahi yako mema. Mungu anakupenda na ana hamu ya urafiki nawe!


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba umeahidi kuwa rafiki yangu. Nisaidie kuja kwako kwa maombi, nikijua kuwa unanipenda na wewe unanijali. Asante, Mungu, kwamba huwa siwi peke yangu. Wewe ni rafiki yangu, na uko nami.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon