Umuhimu wa kuwatendea Wengine Mema

Umuhimu wa kuwatendea Wengine Mema

Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi… —WAEFESO 4:30

Ninachukua msitari kama Waefeso 4:30 kwa uzito kabisa—bila shaka sitaki “kumhuzunisha Roho Mtakatifu” na ninajua usingependa pia. Lakini tunaweza kuepuka vipi kufanya hivyo?

Kusoma mistari inayozunguka msitari wa 30 inaweka wazi kwamba kitu kimoja kinachomhuzunisha Roho Mtakatifu ni wakati ule watu wanatesana. Fikiria kwamba:

  • Katika msitari wa 29 tunahimizwa kuinua wengine kwa maneno au kwa midomo yetu.
  • Msitari wa 31 unatusihi tusiwe wenye uchungu, hasira au ushindani, na kujihadhari na uzushi, chuki na nia mbaya.
  • Katika msitari wa 32 tunaambiwa tuwe wenye huruma kwa wengine, na kusamehe kwa utayari na uhuru.

Tunapotambua kwamba inamhuzunisha Roho Mtakatifu tunapokuwa wenye chuki au ugomvi na mtu, au tukishinda tukiwa tumekasirika, itabidi tubadilike.

Ninakuhimiza kumwomba Mungu akusaidie kuona wengine jinsi anavyowaona. Mwombe akupe huruma na uvumilivu unaohitaji ili kukabiliana kwa upole na upendo na watu walio katika maisha yako, haswa wale wasio na huruma na ni wagumu kuwa karibu nao. Mungu atafurahi atakapoona kwamba una nia ya moyo wa kutaka kuwapenda na kuwabariki watu wengine.


Mojawapo ya siri muhimu ya kuwa na furaha ni kutembea katika upendo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon