Adui pia ana mpango

Adui pia ana mpango

Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. 1 Petero 5:8

 Mungu ana mpango wa maisha yako, lakini shetani ana mpango na wewe pia. Kwa hivyo Biblia inasema tunahitaji kuwa na uwiano mzuri (mwangalifu, akili makini), kuwa macho na tahadhari wakati wote.

Maana ya kiasi ni “nidhamu,” maana ya  umakinifu ni “kuwa mwangalifu,” kuwa macho ina maana “kukata kauli” na maana ya tahadhari ni “makini.”

Tunapaswa kuishi hivi wakati wote. Hiyo ni kubwa. Lakini tunahitaji kumaanisha ili kupigana na adui. Wakati wowote Mungu akionyesha eneo lolote katika maisha yako ambapo adui anakushambulia, huo si wakati wa kukaa nyuma na kutofanya chochote. Ni wakati wa kuamua na kupigana dhidi ya Shetani.

Mpango wa Mungu kwetu ni kuwa zaidi ya washindi katika Kristo. Hatuhitaji kuishi kama watumwa wa mpango wa adui. Unaweza kuamua hivi sasa kufanya kile unachohitaji kufanya. Kata kauli na Mungu, fuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, na uendelee kujihadharini dhidi ya adui. Chagua leo kufuata mpango wa Mungu kwa maisha yako, sio Shetani, na wewe utashinda adui kila upande.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nachagua mpango wako, sio wa adui. Nionyeshe maeneo ambayo ananipiga na unisaidie kumshinda

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon