Amini Tu

Amini Tu

Lakini nachelea kama vile nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikra zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. 2 WAKORINTHO 11:3 BIBLIA

Mpango wa Mungu juu yetu kwa kweli ni rahisi sana kiasi cha kwamba mara nyingi huwa tunaukosa. Yesu ametuambia cha kufanya ili kuanza kutambua mpango wa Mungu: Amini! (tazama Yohana 1:12; 3:16)

Mungu anapokuambia kitu katika moyo wako, au unaposoma kitu katika Biblia, unafaa kusema: “Asante Bwana. Ninaamini. Mungu akisema atanifanikisha, ninaamini (tazama Yeremia 29:11). Mungu akisema nitavuna ninachopanda, ninaamini (tazama 2 Wakorintho 9:6). Akisema niombee adui zangu, ninaamini, na nitafanya hivyo (tazama Mathayo 5:44). Akisema nitaje yale yasiyokuwako kama kwamba yamekuwako, ninaamini, na nitafanya (tazama Warumi 4:17 Biblia).”

Ukichagua kuanza kuamini Neno la Mungu, hata kabla ya kuona hali zako zikibadilika, basi utakuwa na furaha. Amini Mungu tu!


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kurahisisha vitu leo kwa kuamini tu Neno lako. Asante kwa ahadi ambazo umenipa kama mwanao. Leo ninachagua tu kuamini kuwa yale uliyoyasema ni ya kweli katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon