Toa upendo unaoweka huru

Toa upendo unaoweka huru

Basi ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.  2 Wakorintho 3:17

Upendo huleta  uhuru. Huleta hisia ya kukubalika na hisia ya uhuru. Upendo haujaribu kudhibiti au kudanganya wengine au kufikia utimilifu kupitia hatima ya wengine.

Yesu alisema kwamba alitumwa na Mungu kutangaza uhuru. Kama waumini, ndio tunachotakiwa kufanya pia-kuwapa watu uhuru wa kutimiza mapenzi ya Mungu kwa maisha yao, si kuwaleta chini ya udhibiti wetu.

Nimegundua kuwa kujaribu kuwafanya watu kufanya kile ambacho mimi nataka wafanye huzuia mlango kwa Mungu kuwa na uwezo wa kuzungumza na mioyo yao. Tunahitaji kuwaacha watu katika maisha yetu kuwa yote wanayoweza kuwa kwa utukufu wa Mungu, sio wetu wenyewe.

Weka watu huru na watakupenda. Usiwe na udanganyifu. Badala yake, jifunze kumruhusu Mungu awe na udhibiti wa maisha yao. Mtu mwenye upendo mkubwa ni mtu ambaye anaweza kuachilia watu na vitu. Leo, usiwe mtu anayedhibiti, lakini anayepeana kwa uhuru upendo wa ukombozi ambao hutoka tu kwa Mungu.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nataka upendo ninaowapa wengine kuwa sawa na uhuru wa upendo unaowapa. Ninaacha tamaa yangu ya kudhibiti na kuongoza. Nitawapenda tu wale unaowaweka katika maisha yangu na kuwapeana kwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon