Lijue neno kwa ajili yako mwenyewe

Lijue neno kwa ajili yako mwenyewe

Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. 1 Yohana 2:14

Ikiwa umekuwa unashangaa kwa nini daima inaonekana kuwa wewe unapitia kitu-unakabiliwa na tatizo moja au nyingine – na hauna ushindi katika maisha yako, huenda ukahitaji kutumia muda mwingi kukaa katika Neno. Waumini wengi huenda kanisa kila wiki ili kusikiliza mtu mwingine akiwahubiri Neno, lakini hawajui Neno kwao wenyewe.

Ikiwa unataka kuishi katika ushindi, lipe Neno la Mungu nafasi ya kipaumbele katika maisha yako ya kila siku. Kwa kawaida, hii inaweza kumaanisha kukiri Neno wakati unapojitayarisha asubuhi, au kusikiliza mafundisho au kuabudu na muziki unapofanya kazi. Unaweza kutumia saa yako ya chakula cha mchana kusoma Neno au kutembea nje na kuomba.

Haya ni mawazo machache tu ya kuunganisha Neno la Mungu katika maisha yako. Fanya kile kinachofaa kwako ili uhakikishe unafuata ukweli Wake kwa msingi, unapoendelea na maisha yako. Kulipa Neno Lake nafasi ya kipaumbele kutabadilisha maisha yako.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nataka kuunganisha kikamilifu Neno lako katika maisha yangu. Sitaki tu kusikia mtu akiniambia Neno mara moja kwa wiki, nataka kujua mwenyewe. Niongoze na unionyeshe njia za kufuata Neno lako mara kwa mara.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon