Kushugulika na kukata tama

Kushugulika na kukata tama

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Yakobo 4:7

Wakristo wengi wamesalia kwenye njia panda ya maisha huku wamevunjika moyo na huzuni kwa sababu hawajajifunza jinsi ya kukabiliana na hali ya kukata tamaa. Lakini sio mapenzi ya Mungu kwako kuishi maisha ya kukata tamaa, huzuni au kushushwa moyo leo-au siku yoyote.

Sehemu ya utumishi wa Yesu wa duniani ilikuwa ni kwenda katika kuwapaka watu mafuta ya Roho Mtakatifu na kuwaokoa wale wote waliodhulumiwa na shetani. Watu waliopotea kila mahali walipata tumaini jipya walipokutana na nguvu za Yesu. Nguvu hiyo hiyo inapatikana kwetu leo. Tumia nguvu hiyo kujitetea dhidi ya kukata tamaa kwa kuzingatia Mungu, kutafakari juu ya ahadi zake, kukiri Neno Lake, na kujitoa mwenyewe na hali yako kwa Yeye katika sala.

Kupitia Yesu, unaweza kupambana na jitihada za adui kukupima, kumkemea ili asiweze kukuharibu. Wakati shetani anafanya hatua moja kuelekea kwako, unaweza kumakinika  kiroho na utaweza kutambua kile anajaribu kufanya, kumpinga na kumsababisha kukimbia. Kwa nguvu ambazo Yesu alikuwezesha, hana chaguo bali kukimbia

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, matatizo na mambo ya kukata tamaa yatafika kwa njia yangu, lakini siwezi kukata tamaa. Ninapoendelea kukubiliana na Wewe, nitampinga shetani na kumkimbisha kila wakati.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon