Baba Yako Anataka Kuzungumza Nawe

[Roho ambaye] si roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia Aba yaani Baba (WARUMI 8:15)  

Roho Mtakatifu ni Roho wa kuasili. Hii ina maana kwamba kwa nguvu za Roho Mtakatifu, kwa kweli sisi ni sehemu ya familia ya Mungu. Tulikuwa watenda dhambi wakati mmoja tukimtumikia shetani, lakini Mungu akatukomboa, akatununua kwa damu ya Mwanawe, na hutuita wanawe wapendwa wa kike na kiume.

Uasilishaji ni wa ajabu! Mtu anayetaka mtoto hukusudia kuchagua mmoja na kumchukua kama wake kumpenda na kumtunza. Katika hali zingine, hii inaweza kuwa bora zaidi kuliko kuzaliwa katika familia ambayo inawakataa. Wakati mwingine kuzaliwa huko hutokana na uteuzi ambao wazazi hujuta kufanya. Lakini watoto wakiasiliwa, wanatakiwa, kuteuliwa maalum, na kuchaguliwa kimakusudi.

Tunapochagua kuweka imani yetu ndani ya Yesu Kristo, kuzaliwa huko kupya hutuleta katika familia ya Mungu. Anakuwa Baba yetu; tunakuwa warithi wa Mungu na warithi pamoja na Yesu (soma Warumi 8:16-17). Anatushughulikia kama Baba mtimilifu na mwenye upendo. Baba mwema si mnyamavu kwa wanawe. Huwafanyia vitu vingi, vile tu Mungu hutufanyia, hata kuzungumza nao ili kuwaambia jinsi anavyowapenda, kuwaagiza, kuwaongoza, kuwaonya, kuwapa hakikisho, na kuwahimiza. Wewe ni wa Mungu; amekuasili na sasa ni Baba yako; na anataka kuzungumza nawe leo. Iwapo umekuwa na tajriba chungu ya kukataliwa au kutelekezwa na wazazi wako, acha nikukumbushe kwamba Mungu hukuasili na kukuchukua kama mtoto wake mwenyewe (soma Zaburi 27:10).

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu anafikiri wewe ni mtu maalum. Amekuchagua kuwa mtoto wake mwenyewe.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon