Matumaini: Matarajio yenye furaha ya mambo mema

Matumaini: Matarajio yenye furaha ya mambo mema

Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima. Mithali 13:12

Ninafafanua tumaini kama “matarajio ya furaha ya mambo mazuri.” Tunapotarajia wema wa Mungu katika maisha yetu, hii hufungua mlango wa furaha zaidi. Hivyo je, wewe unatarajia sana kitu kizuri kikufanyikie?

Mradi tunaishi, sote  tutaendelea kwenda mahali fulani. Mungu alituumba kuwa wenye maono na wenye lengo. Bila maono, tunakuwa wachovu na kukosa tumaini.   Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua, kulingana na Mithali 13:12 Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.

Mungu anataka tuishi kwa tumaini lake ili tuweze kufurahia maisha.

Huwezi kuwa na furaha ikiwa huna tumaini. Kadri unavyozidi kuwa na tumaini katika Mungu, ndivyo furaha yako itazidi. Matumaini inaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa kabisa.

Ili kufurahia maisha unapaswa kudumisha mtazamo mzuri wa matumaini. Mungu ana mtazamo chanya, na anataka vitu vyema kutokea kwa kila mmoja wetu, hivyo jijaze na matumaini Yake leo na uendelee na matarajio yenye furaha ya mambo mema.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, mimi nafanya uchaguzi leo kuwa na furaha ya kutarajia wema wako katika maisha yangu. Na kama matumaini yangu yataongezeka, najua furaha yangu itaongeza pia. Bwana, ninaweka tumaini langu ndani yako!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon