Baraka Kuu

Baraka Kuu

Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma yake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. —1 YOHANA 3:17–18

Njia rahisi kabisa ya kubarikiwa ni kuamua kuwa baraka kwa wengine. Unapochagua kuwa na moyo mkarimu ambao unawasaidia wengine kwa kukutana na mahitaji yao, Mungu humwaga upaji wake katika maisha yako. Mtu ambaye ni mto wa baraka huwa hakauki.

Kitu ndani kabisa ya moyo wa aaminiye kinataka kuwasaidia wengine. Hata hivyo ubinafsi unaweza kutuzuia vikali kushughulikia tamaa zetu hata tukakosa kutambua mahitaji ya wale wanaotuzunguka.

Watu wanadhurika kila mahali. Wengine ni maskini; wengine ni wagonjwa au pweke. Bado wengine wamejeruhiwa kihisia au wana mahitaji ya kiroho. Kitendo rahisi cha ukarimu kwa mtu aliyedhurika kinaweza kumfanya huyo mtu akahisi kupendwa na kuthaminiwa.

Watu wanaweza kushikika katika mtego wa kung’ang’ana kuwa na vingi zaidi na zaidi. Kung’ang’ana huko huzalisha matokeo machache au hata yakakosa kuwepo. Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kung’ang’ana kushinda katika kuwasaidia wengine. Tutakapofanya hivi, tutapata kwamba Mungu atahakikisha tuna vya kutosha vya kukutana na mahitaji yetu wenyewe na vingi vya kutoa.


Hakuna baraka kuu kuliko kuwapa wengine walio na mahitaji.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon