Wabarikini wanaowaudhi; barikini wala msilaani. —WARUMI 12:14
Mungu katika Neno lake anatuagiza kusamehe wengine halafu kuwabariki. Katika Warumi 12:14, neno bariki linamaanisha “kusema vizuri kuhusu.” Ni kuwaonyesha rehema kwa watu ambao huenda hata hawastahili. Na kuwaombea ili wabarikiwe. Tunahitajiwa kuomba Mungu awape ukweli na ufunuo kuhusu mabadiliko yoyote wanayohitaji kufanya katika mielekeo na tabia zao, na kuwasaidia kuja mahali pa toba ili wawekwe huru kutokana na dhambi zao.
Kisasi husema, “Ulinitesa, kwa nami nitakutesa pia.” Rehema husema, “Ulinitesa, kwa hivyo nitakusamehe, kukurejesha, na kuingiliana nawe kama ambaye hujawahi kunikosea.” Baraka ilioje kuweza kutoa na kupokea rehema. Toa rehema na utapokea rehema.
Rehema ni sifa ya Mungu ambayo huonekana katika vile anavyoshughulikia watu wake. Rehema hutukaribia tunapostahili kufukuzwa. Rehema ni nzuri kwetu tunapostahili hukumu. Rehema hutukubali na kutubariki tunapostahili kukataliwa kabisa. Rehema huelewa udhaifu wetu na haituhukumu.
Kwa kweli iwapo tunafurahia rehema ambayo Mungu ametuonyesha, tutakuwa wepesi wa kutoa rehema hiyo hiyo kwa watu wengine.
Nguvu za msamaha hazitawahi kufanya kazi iwapo tutasema tunasamehe lakini tena kurudi nyuma na kulaani waliotukosea kwa ulimi au kuwaambia wengine kuhusu makosa hayo.