Endelea Kutembea

Endelea Kutembea

Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji ili kumwendea Yesu. —MATHAYO 14:28–29

Petro alipotoka katika mashua kwa amri ya Yesu, alikuwa anafanya kitu ambacho hakuwahi kufanya. Alipoendelea kuwa na imani alifanikiwa, lakini hofu ilipouvaa moyo wake, alianza kuzama!

Makosa ya Petro ni kwamba alianza kushughulika na mawimbi. Alipowaza kuhusu hali iliyomzingira, badala ya Mwokozi aliyekuwa karibu naye, alipoteza imani yake na kuanza kushuku.

Warumi 4: 18- 21 inatuambia kuwa Ibrahimu hakuyumbayumba katika imani yake alipokabiliwa na hali ngumu. Aliitambua hali yake, lakini kinyume na Petro, hakuiwaza. Ni imani yake ya ukakamavu na kulenga mbele iliyomsukuma mbele.

Ninaamini kwamba mimi na wewe tunaweza kujifunza kutokana na makosa ya Petro na mfano wa Ibrahimu. Tunaweza kutambua hali zetu lakini tusiziwaze. Tunaweza kuweka mawazo yetu kimaksudi juu ya Yesu, tukimtumainia kwa imani kwamba atatupatia muujiza tunaohitaji.


Mawimbi yanapokuja katika maisha yako, mtazame Yesu na ukusudie kutembea naye bila kujali kimo cha mawimbi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon