Fanya Ukiwa na Woga

Bwana akamwambia Abramu, toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha. —MWANZO 12:1

Utahisi vipi iwapo Mungu atakuambia kutoka kwenu, kuacha familia yenu, na kila kitu ulichozoea na kinachokuridhisha na kwenda usikojua. Utakuwa mwoga? Hiyo ndiyo haswa changamoto iliyomkabili Abramu, na ikamtia hofu. Ndiyo maana kila mara Mungu alikuwa akimwambia, “Usiogope.”

Elisabeth Elliot, ambaye mume wake aliuwawa pamoja na wamishenari wengine nchini Ecuador, anasema vile maisha yake yalivyodhibitiwa na hofu. Kila wakati alipotaka kufanya kitu, woga ulimzuia hadi rafiki yake akamwambia kitu kilichomweka huru. Alisema, “Kwa nini usikifanye ukiwa na woga?” Elisabeth Elliot na Rachel Saint, dadake mmojawapo wa wamishenari waliouawa, alianza kufanya uinjilisti miongoni mwa makabila ya Kihindi, wakiwemo watu waliowaua mume na kaka wao.

Tukingoja kufanya kitu saa ile hatuna woga, tutamtimizia Mungu machache sana, na wengine pia au hata sisi wenyewe. Iliwabidi Abramu na Yoshua kuchukua hatua ya imani na utiifu kwa Mungu ili kufanya walioamriwa na Mungu kufanya—hata kama walihisi woga. Tunaweza kufanya vivyo hivyo!


Amua kuwa maisha yako hayatatawaliwa na woga bali na Neno la Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon