Je, unadhani Mungu anapenda vazi moja badala ya lingine?

Je, unadhani Mungu anapenda vazi moja badala ya lingine?

Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.  1 Samweli 16:7

 Nilikuwa nikihukumu sana kuhusu njia ambazo watu wengine wamevaa. Nilikuwa nadhani kwamba sipaswi kuvaa jeans wakati nilipofundisha kwenye mkutano, lakini mtoto wangu aliniambia, “Je, unafikiri kweli kwamba Mungu anapaka mafuta vazi moja badala ya lingine?”

Ilichukua mambo kama hayo ya kunishutumu kutambua kwamba nilikuwa nimezingatia hali ya kidini wakati Mungu alitaka nipate kuwa mwangalifu ili kufikia watu wengi. Hakika, ni vizuri kuvaa vizuri wakati tunapokuja kanisani. Lakini mstari wa msingi ni, hatupaswi kuzingatia uonekano wetu wa nje kiasi kwamba tunapoteza lengo letu kuu: kuendeleza uhusiano wa karibu na wa kibinafsi na Mungu.

Mungu anataka sisi tushirikiane naye, ambayo inamaanisha kuwasiliana naye katika siku zetu tu kama tunavyofanya na mtu ambaye ni rafiki yetu wa karibu au wa familia. Hajali juu ya kuonekana kwa nje … ila uhusiano wa kweli. Tumia wakati pamoja Naye, kuwa na shukrani kwa kile alichofanya na anafanya katika maisha yako. Uwe na uhusiano wa kweli naye.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nisaidie kuwa na mtazamo wako juu ya kuonekana nje. Nisaidie nisiwahukumu wengine ambao hawavai kwa njia ambayo nadhani wanapaswa, na unisaidie kuendeleza uhusiano wa ndani na wewe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon