Fungua Mlango

Tazama nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami (Ufunuo 3:20)

Nilipofungua mlango wa moyo wangu kwa ukamilisho wa huduma ya Roho Mtakatifu katika maisha yangu, alianza kuzungumza nami na kushughulika nami kuhusu kila eneo la maisha yangu; hakuna kitu ambacho hakuhusika nacho. Nilipenda hivyo lakini pia sikupenda hivyo iwapo unajua ninachomaanisha.

Mungu akazungumza nami kuhusu vile nilivyozungumza na watu na kuwahusu. Alizungumza kuhusu vile nilivyotumia pesa zangu, nilivyovaa, marafiki zangu na nilichofanya kama burudani. Alizungumza nami kuhusu fikra zangu na nia zangu. Nilitambua kwamba alijua siri zangu za ndani na hakuna kitu kilichofichika mbele zake. Hakuwa tena kwa “chumba cha Jumapili asubuhi” ya maisha yangu, lakini akaonekana kama ambaye alikuwa akidhibiti nyumba nzima! Sikujua wakati ambao angeanza kunizungumzia kuhusu kitu katika maisha yangu. Kama nilivyotaja, hatua hii ilisisimua, lakini ilikuwa pia ya kutia changamoto kwa sababu nilijua kunizungumzia kwake kutaleta mabadiliko mengi katika maisha yangu.

Sisi wote tunataka mabadiliko katika maeneo fulani, lakini yakija, yanaweza kuogofya. Mara nyingi huwa tunataka maisha yetu yabadilike lakini si mienendo yetu ya maisha. Huenda tusipende tulichonacho maishani, lakini huwa tunashangaa kama kinaweza kuwa kizuri kuliko hivyo vibadala. Tunaweza kuhangaika au hata kuwa na wasiwasi wa kupoteza udhibiti wa maisha yetu na kuruhusu mtu tusiyemwona kushika usukani.

Kusikia na kutii sauti ya Mungu anapofanya kazi katika maisha yetu inamaanisha kuishi kwa sababu ya kumpendeza na utukufu wake, sio wetu. Huenda tukaogopa au kuwa na wasiwasi kuhusu kufungua milango ya kila eneo la maisha yetu kwake, lakini ninakuhakikishia kwamba inastahili.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Alika Mungu katika kila eneo la maisha yako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon