Jifunze kusubiri

Jifunze kusubiri

Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. Isaya 40:31

Mara nyingi watu wananiuliza, “Ninawezaje kujua kwa hakika kama ninasikia kutoka kwa Mungu au ninafanya tu mambo yangu?”

Naamini jibu ni kujifunza kusubiri. Kwa maamuzi makubwa, mara nyingi tuna haja ya haraka. Tunapaswa kufanya kitu na kufanya hivi sasa! Lakini hekima ya Mungu inatuambia kusubiri hadi tuwe na picha wazi ya kile tunachotakiwa kufanya na wakati tunapaswa kufanya hivyo.

Sisi sote tunahitaji kuendeleza uwezo wa kuchukua hatua moja nyuma na kuona kila hali kutokana na mtazamo wa Mungu. Basi tunaweza kufanya maamuzi kwa njia ambayo anataka.

Nguvu inapatikana katika kusubiri. Unapomngojea Bwana, unaweza kuelewa katika roho yako kile ambacho Bwana anataka ufanye … sio kile unafikiri anataka ufanye. Unapokabiliwa na uamuzi wowote mgumu, ni busara kusubiri mpaka uwe na jibu wazi kabla ya kuchukua hatua usije kujuta. Unaweza kusikia wasiwasi na ungependa kuharakisha, lakini usiruhusu shinikizo hilo liendelee juu ya hekima na ujuzi wa Mungu.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, sitaki kujipata katika hali ya sintofahamu wakati nitakapofanya uamuzi nije nikajuta. Nikumbushe kukungoja kila siku. Inaweza kuwa vigumu, lakini napokea hekima yako na ujuzi ambayo ni ya thamani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon