Kudhitibi hisia zako

Kudhitibi hisia zako

Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Sefania 3:17

Kushughulika na hisia ni ukweli wa maisha. Tunapoishi, tutapata hisia mbalimbali, na hatupaswi kukataa kuwepo kwao au kujisikia wenye hatia kwa sababu hiyo.

Hata hivyo, tunahitaji kujifunza kusimamia hisia zetu. Hii ni rahisi tukielewa kuwa hatuwezi kuziamini. Kwa kweli, zinaweza kuwa adui yetu mkubwa zaidi. Shetani anatumia hisia zetu dhidi yetu kutuzuia kutembea katika Roho.

Ni muhimu sana kujua kwamba Bwana wetu Mungu ambaye anaishi ndani ya kila mmoja wetu ni mwenye nguvu. Nguvu zake ndani yetu zinatuwezesha kuondokana na hisia zetu na kuongozwa na Neno na Roho Wake badala ya hisia zetu zisizo na uhakika.

Utulivu wa kiroho na ukomavu wa kihisia havikuji kwa kawaida. Lazima uitamani kwa moyo wako wote na ujithamini kupata hiyo. Unapofanya utulivu wa  kihisia kipaumbele, Mungu yuko tayari kukusaidia kusimamia hisia zako.

Ninawahimiza kufuata hayo leo. Kufurahia utulivu wa kihisia na maisha ya ushindi na ya furaha!

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, mimi nachagua kufuata utulivu wa kihisia. Sitaki kudhibitiwa na hisia zangu, lakini nataka kujifunza kusimama vizuri. Asante kwa kuishi ndani yangu na kunisaidia kwa nguvu zako tele

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon