Hakuna Kingine Kinachoridhisha

Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; naam kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema (ISAYA 26:9)

Ulimwengu hufanya iwe rahisi kwetu kujaza masikio yetu na kila aina ya vitu ambavyo huzamisha sauti ya Mungu na kumsukuma mbali, mbali nyuma ya maisha yetu. Hata hivyo, siku huja kwa kila mmoja ambapo Mungu peke yake hubaki. Kila kitu katika maisha hatimaye hupita; na ikiwa hivyo Mungu atakuwa bado yupo hapo.

Biblia inafundisha kwamba, kinachojulikana na Mungu ni dhahiri kw awote kwa sababu amefanya ajulikane katika dhamiri ya ndani ya mwanadamu (soma Warumi 1:19-21). Kila mmoja atasimama mbele zake siku moja na kutoa maelezo ya maisha yake (soma Warumi 1:14:12). Watu wanapokataa kumtumikia Mungu na maisha yao, wanapotaka kwenda katika njia zao wenyewe, wanatafuta njia za kupuuza na kujificha kutokana na maarifa ya Muumba wao anayetaka kuzungumza nao na kuwaelekeza katika njia wanayofaa kwenda.

Ukweli ni kwamba, hata watu wakijaribu kujificha Mungu wala la, hakuna kinachoweza kuridhisha matamanio yetu kwake isipokuwa umoja na ushirika naye. Hata watu wakijaribu kumpuuza, ndani kabisa wangependa kusikia sauti yake.

Ninakuhimiza kuridhisha matamanio yako ya Mungu kwa kutumia muda wako naye, ukiwa umekaa katika uwepo wake, na kusikiliza sauti yake.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Ishi maisha yako kwa njia ambayo huna hofu au woga wa kusimama mbele za Mungu wakati ambao maisha yako duniani yameisha.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon