Huru

Huru

. . . Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote… —1 JOHN 2:1–2

Kuna wakati katika maisha yangu ambapo, ungeniuliza, “Ulifanya kitu gani kibaya mwisho?” Ningetoa maelezo ya kina ya wakati ambao nilikifanya na wakati ambao nilikilipia kwa kujihukumu. Nilishikwa na wasiwasi kuhusu kila kosa dogo nililofanya na kujaribu kujizuia kutenda dhambi bila mafanikio. Hadi nilipoelewa msamaha wa Mungu ndipo nikawa huru kutokana na kujichunguza ambako kulifanya maisha yangu yawe magumu sana.

Ukiamini kwamba lazima uwe mtimilifu ndipo upendwe na kukubalika, basi utasikitika maishani kwa sababu hutawahi kuwa mtimilifu mradi tu baada uko katika mwili wa udongo. Kadri unavyomkaribia Mungu, ndivyo unatambua kwamba anakupenda hata katikati ya kutokutimilika kwako. Usijilaumu. Mungu huona moyo wako—kiasi kwamba matamanio yako ni kumpendeza katika vitu vyote—lakini matendo yako hayawezi kuwiana na matamanio ya moyo wako hadi utakapofika mbinguni. Unaweza kuendelea kuboreka kila wakati na kuchuchumilia mbele hadi kwenye kiwango cha utimilifu, lakini utahitaji rehema na msamaha wa Yesu wakati wote.


Jibu la Mungu kwa kutotimilika kwetu ni msamaha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon