Imani na Kibali

Mwenendo wa Mungu watoka kwa Bwana. Basi awezaje mtu kuelewa njia zake? (MITHALI 20:24)

Wakati mimi na Dave tulihisi Mungu akituita kuanzisha huduma ya televisheni, tulianza kuchukua hatua tukielekea huko kwa imani. Hatungeweza bila pesa, kwa hivyo jambo la kwanza tulilofanya lilikuwa kuwaandikia watu waliokuwa katika orodha yetu ya barua, kuwaambia marafiki na washiriki wa huduma kutoa fedha ili kutusaidia kuanzisha huduma ya televisheni. Tulihisi Mungu alikuwa amezungumza na mioyo yetu kuhusu kiasi fulani cha fedha ambacho tungehitaji ili kuanzisha na hicho kiasi ndicho tulipokea haswa.

Halafu tukachukua hatua nyingine. Tulihitaji mzalishaji na Mungu akamleta. Mtu alikuwa ametuma maombi ya kazi ya uzalishaji wa televisheni miezi mitatu kabla Mungu atunenee kuhusu kuwa kwenye runinga. Kwa vile hatukuwa kwenye televisheni, tulimwambia hatutahitaji huduma zake. Wakati ulipokuja, tulimkumbuka mtu huyo na tukatambua kwamba Mungu alikuwa amekutana na hitaji letu hata kabla tujue tulikuwa nalo.

Hatua nyingine tuliyochukua ni kununua wakati wa kupeperusha kipindi chetu kwenye vituo vichache mara moja kwa wiki. Vipindi hivyo vilipojilipia vyenyewe na tukaona matunda mazuri kutokana navyo, tulinunua wakati zaidi. Hatimaye tukaanza kupeperusha kila siku, na sasa tuna kipindi cha kila siku ambacho hupeperushwa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu na kwa maombi kinasaidia mamilioni ya watu.

Mungu alimwongoza Dave na mimi hatua moja baada ya nyingine na hivyo ndivyo atakavyokuongoza. Kila wakati tulipochukua hatua ya imani, Mungu alitupatia kibali, na ninakuhimiza kutarajia kibali pia. Tayari Mungu anajua mahitaji yako na ana jibu lako, kwa hivyo hofu ikibisha kwenye mlango wako, jibu kwa imani na utafanya mambo makuu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kuwa na hakika kwamba Mungu anakuongoza na kukupa kibali.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon