Jisemeshe Maneno Ya Uzima

Jisemeshe Maneno Ya Uzima

Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi, na wao waupendao watakula matunda yake. MITHALI 18:21

Maneno unayosema huamua nia na mtazamo wako juu ya maisha. Ukiamua kwamba utasema maneno machache iwezekanavyo kuhusu shida na masikitiko yako katika maisha, hayatatawala fikra na hali yako ya moyo. Wakati umefika wa kuacha kufikiria shida zetu na kuanza kufikiria kuhusu wema wa Mungu.

Ukiongea sana iwezekanavyo kuhusu baraka na tumaini la matarajio yako kwa nia yenye shukrani, nafsi yako italingana navyo. Hakikisha kwamba kila siku inajaa maneno yanayochochea upendo, amani na furaha, sio hasira, mfadhaiko, uchungu na hofu. Jiambie maneno ya uzima! Tafuta kitu chanya cha kusema katika kila hali, huku ukisalia kuwa mwenye shukrani kwa baraka za Mungu ambazo zimekuzunguka.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa kila baraka uliyonipa. Ninachagua kukutazama wewe na upaji wako katika maisha yangu, badala ya kufikiria shida zangu au mahitaji. Ninajua kwamba utanipa, kwa hivyo mawazo na imani yangu itakulenga wewe na maneno ninayosema pia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon