Kataa Kukasirika

Kataa Kukasirika

Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; nayo ni fahari yake kusamehe makosa. MITHALI 19:11

Tuna nafasi nyingi kila siku za kukasirika; huwa tunalazimika kufanya uteuzi kila wakati. Tukichagua kuishi kwa hisia zetu, hatutawahi kunawiri katika sehemu ya upendo inayoitwa msamaha. Msamaha ndio kiuasumu cha kosa, na tunaweza kushukuru sana kwamba Mungu ametupatia kama njia yetu ya kuwa na amani.

Wakati mmoja nilisoma kwamba asilimia 95 ya wakati ambao watu huudhi hisia zetu, huwa hawakusudii kufanya hivyo. Wakati wote huwa tunaonekana kuchukulia kuwa watu wanatushambulia, ilhali ukweli ni kwamba, labda hawaelewi tu vile tabia yao inavyotudhuru. Ni nadra sana watu kukesha usiku wakipanga vile watawaudhi watu watakaokutana nao siku itakayofuatia. Viwango vya msongo wa mawazo viko juu ulimwenguni leo, na mara nyingi watu hutuumiza moyo kwa sababu ya mshinikizo wanaohisi ndani yao.

“Iachilie, iache, na uache iende,” ndivyo Biblia ya Amplified inavyosema tufanye na hasira (tazama Marko 11:25). Ni muhimu kusamehe haraka. Shukuru kwamba, kadri tunavyosamehe haraka, ndivyo inavyokuwa rahisi kusamehe. Mungu ni upendo, na husamehe na kusahau. Ili tufanane naye, tunaweza kuwa na tabia kama hiyo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba umenisamehe dhambi zangu zote. Ninaomba kwamba unisaidie kufuata mfano wako na kuwasamehe wale watu walioniudhi. Asante kwa nguvu zako ambazo huniwezesha kusamehe wengine na kuishi bila udhia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon