Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu? —LUKA 22:48
Yesu alijitwika dhambi zetu ili tusijitwike sisi wenyewe. Lakini kuna vitu vingine ambavyo alivumilia akiwa njiani kuelekea msalabani na vinaweza kuwa mfano kwetu, vitu ambavyo itatulazimu tupitie na hatua tutakazochukua ili kumfuata. Yesu alikabiliana na usaliti wa Yuda kwa wakati mbaya sana wa maisha yake lakini hakuacha hilo limzuie.
Usaliti ni mchungu haswa tukidhuriwa na mtu tunayependa, kuheshimu, na kutumainia. Huenda tukawa wenye mwelekeo wa kujitetea na wenye uchungu kwa juhudi za kuzuia kudhuriwa tena. Lakini kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kupata uponyaji kutokana na usaliti ili usituzuie, hata kama tutakuwa tunahisi vipi.
Katika Mathayo 24:10-13, Yesu anatuonya kwamba katika siku za mwisho usaliti utaongezeka. Kama waaminio jinsi tunavyokabiliana na watu wanavyotusikitisha ni muhimu kuliko mambo waliyotufanyia. Iwapo umesalitiwa au kudhuriwa na mtu uliyetumainia, kataa kuwa na uchungu.
Badala yake, fuata mfano wa Yesu na uwasamehe. Hatuwezi kuchagua kile watu wengine watatutenda, lakini tunaweza kuchagua kukabiliana nayo kwa usahihi.
Lazima tuamue kwamba kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kuruhusu uchungu wetu kutuboresha, bali si kuwa wenye uchungu.